Petu na Garu PETU NA GARU ni hadithi inayomuhusu Mzee Mambo, ambaye ni dereva taxi katika mji wa Bagamoyo. Mzee mambo anapata taarifa za uhakika za mauaji ya dereva taxi mwenzao ambaye anaitwa Pondamali. Maiti ya Pondamali ilikutwa ikining’inia katika mti, kuashiria kuwa amejinyonga mwenyewe.