Baada ya kufeli mitihani ya kidato cha nne na kulazimishwa kuolewa na wazazi wake, Edina anakataa kukubali kushindwa. Akiwa mama mchanga, anaanza safari ya kujipambania upya, akirudi shule na kuanzisha biashara ndogo. Katika changamoto zote, anasimama imara na kuwa mkombozi wa familia yake, hasa pale mumewe alipokosa mwelekeo. Ni hadithi ya ujasiri na matumaini, ikionyesha kuwa ushindi unaweza kupatikana hata kwenye mazingira magumu zaidi.
Maturity Level : all
Ngonya alizaliwa chini ya mti wa mikutano ya wachawi, na baada ya mama yake kufariki, wachawi walimlea wakimwandaa kuwa kiongozi wao. Alikua akikabiliana na vitisho vya uchawi huku akikataa hatima hiyo ya giza. Tobi na Mike walijaribu kupambana na nguvu za wachawi, huku Mika akiongoza jitihada za kuangamiza uchawi kijijini. Ngonya alipitia changamoto nyingi, kama kumpoteza Hance kwa mizimu na kushuhudia marafiki wakipoteza maisha kutokana na vitisho vya wachawi. Hatimaye, Mika na wenzake waliangamiza wachawi kwa kuteketeza mkoba wa uchawi. Hance alirudi mjini, na Tobi alimwomba Ngonya msamaha baada ya kugundua Ngonya akuwa mchawi.
Maturity Level : 16_plus
Vuguvugu la Imani ni tamthilia inayosimulia Malkia wa kuzimu, aliyekuwa mwanadamu kabla ya kifo chake. Baada ya kifo, alikabidhiwa wadhifa mkubwa na majini katika ulimwengu wa siri na kupewa jukumu la kuwaadhibu wanaume wenye tabia za uzinifu. Wakati Mzee Otako na wengine wanakumbwa na hatari, mke wa Mzee Otako anamtafuta Mama Mchungaji ili amuombee mumewe na kumsaidia kupambana na viumbe hawa wa ulimwengu wa siri. Mwisho, Mama Mchungaji anaweza kuwashinda viumbe hao, Mzee Otako anaomba msamaha kwa mke wake, na kisha wanaendelea na maisha yao kwa amani.
Mwali Kakua ni simulizi ya kusisimua inayochunguza athari za utandawazi kwa familia na tamaduni. Inahusu safari ya binti kijana anayekua ghafla, akikabiliana na changamoto za maisha mapya huku akijaribu kushikilia maadili aliyofundishwa na wazazi wake. Hadithi yenye maswali ya kina kuhusu kizazi kipya na urithi wa tamaduni zetu.
Kunanini kilicho jificha nyuma ya pazia? Maisha ya mastaa tunayoyaona kwenye mitandao mara nyingi hujaa tabasamu, safari za kifahari na furaha isiyoisha. Lakini je, hiyo ndiyo hali halisi ya maisha yao? Nyuma ya kamera kuna simulizi nyingine tofauti—changamoto, mapambano ya ndani, na wakati mwingine upweke unaofichwa kwa umakini. Je, maisha yao ya mitandaoni yanaendana kweli na uhalisia? Hii ni safari ya kugundua majibu ya maswali uliyokuwa nayo kwa muda mrefu. Sasa pazia linafunguka, na ukweli unawekwa wazi ndani ya Superstar
Baada ya uporaji wa dhahabu kwenda vibaya mjini Arusha, kundi la wezi wanawake linaloongozwa na Diva linajikuta likikimbilia Dar es Salaam likitafuta usalama na mwanzo mpya. Wakiwa na kile wanachoamini kuwa ni dhahabu halisi waliyoiba kutoka kwa jambazi sugu, Jitu, wanaamini wamepata tiketi ya kuokoa maisha yao. Lakini wanapofika jijini, matumaini yao yanayeyuka haraka. Mwenyeji wao anaporwa kikatili, na ukweli unaofichuka unawavunja nguvu: dhahabu yao ni bandia, na Jitu tayari amewafuata jijini akiwa na kiu ya kisasi. Wakiwa kifukara na bila mwelekeo, Diva na timu yake wanalazimika kukubali mpango wa ushirikiano na Twaha, mtawala wa eneo hatari la mitaa ya Dar es Salaam. Pasipo wao kujua, Twaha na watu wake ndio waliosababisha mkasa uliowapotezea kila kitu. Ushirikiano huu wa kulazimishwa unawaingiza wasichana hao kwenye mtandao mpana wa magenge, usaliti, na vita ya madaraka. Wakati Jitu anapofanikiwa kuwakamata, msaidizi wa Twaha anaongoza oparesheni ya uokoaji wa kushtukiza, ikibadilisha uhusiano kati ya pande hizo mbili na kuweka misingi ya muungano mpya wenye madhara makubwa. Diva na Twaha wanaungana na kuanza kutekeleza uhalifu wa kiwango cha juu—kutoka uporaji wa kanisa hadi wizi hatari wa benki—wakijaribu kujijengea hadhi katika ulimwengu wa giza. Lakini kadiri wanavyopanda ngazi ya uhalifu, ndivyo wanavyoivutia macho ya mtu hatari zaidi ya wote: Bwana Tembo, mpelelezi wa kiintelijensia mwenye uwezo wa kufuatilia, kuunganisha matukio, na kubaini udhaifu wa kila mshukiwa bila makosa. Anaanza kuwasonga taratibu, akivunja miungano yao kwa ustadi na kusogeza kitanzi shingoni mwao hatua kwa hatua.
Maturity Level : 18_plus