Nguvu ya Mwanamke Baada ya kufeli mitihani ya kidato cha nne na kulazimishwa kuolewa na wazazi wake, Edina anakataa kukubali kushindwa. Akiwa mama mchanga, anaanza safari ya kujipambania upya, akirudi shule na kuanzisha biashara ndogo. Katika changamoto zote, anasimama imara na kuwa mkombozi wa familia yake, hasa pale mumewe alipokosa mwelekeo. Ni hadithi ya ujasiri na matumaini, ikionyesha kuwa ushindi unaweza kupatikana hata kwenye mazingira magumu zaidi.