Vuguvugu la Imani Vuguvugu la Imani ni tamthilia inayosimulia Malkia wa kuzimu, aliyekuwa mwanadamu kabla ya kifo chake. Baada ya kifo, alikabidhiwa wadhifa mkubwa na majini katika ulimwengu wa siri na kupewa jukumu la kuwaadhibu wanaume wenye tabia za uzinifu. Wakati Mzee Otako na wengine wanakumbwa na hatari, mke wa Mzee Otako anamtafuta Mama Mchungaji ili amuombee mumewe na kumsaidia kupambana na viumbe hawa wa ulimwengu wa siri. Mwisho, Mama Mchungaji anaweza kuwashinda viumbe hao, Mzee Otako anaomba msamaha kwa mke wake, na kisha wanaendelea na maisha yao kwa amani.