Mwali Kakua ni simulizi ya kusisimua inayochunguza athari za utandawazi kwa familia na tamaduni. Inahusu safari ya binti kijana anayekua ghafla, akikabiliana na changamoto za maisha mapya huku akijaribu kushikilia maadili aliyofundishwa na wazazi wake. Hadithi yenye maswali ya kina kuhusu kizazi kipya na urithi wa tamaduni zetu.
Maturity Level : 16_plus
Vuguvugu la Imani ni tamthilia inayosimulia Malkia wa kuzimu, aliyekuwa mwanadamu kabla ya kifo chake. Baada ya kifo, alikabidhiwa wadhifa mkubwa na majini katika ulimwengu wa siri na kupewa jukumu la kuwaadhibu wanaume wenye tabia za uzinifu. Wakati Mzee Otako na wengine wanakumbwa na hatari, mke wa Mzee Otako anamtafuta Mama Mchungaji ili amuombee mumewe na kumsaidia kupambana na viumbe hawa wa ulimwengu wa siri. Mwisho, Mama Mchungaji anaweza kuwashinda viumbe hao, Mzee Otako anaomba msamaha kwa mke wake, na kisha wanaendelea na maisha yao kwa amani.
Ngonya alizaliwa chini ya mti wa mikutano ya wachawi, na baada ya mama yake kufariki, wachawi walimlea wakimwandaa kuwa kiongozi wao. Alikua akikabiliana na vitisho vya uchawi huku akikataa hatima hiyo ya giza. Tobi na Mike walijaribu kupambana na nguvu za wachawi, huku Mika akiongoza jitihada za kuangamiza uchawi kijijini. Ngonya alipitia changamoto nyingi, kama kumpoteza Hance kwa mizimu na kushuhudia marafiki wakipoteza maisha kutokana na vitisho vya wachawi. Hatimaye, Mika na wenzake waliangamiza wachawi kwa kuteketeza mkoba wa uchawi. Hance alirudi mjini, na Tobi alimwomba Ngonya msamaha baada ya kugundua Ngonya akuwa mchawi.
Baada ya kufeli mitihani ya kidato cha nne na kulazimishwa kuolewa na wazazi wake, Edina anakataa kukubali kushindwa. Akiwa mama mchanga, anaanza safari ya kujipambania upya, akirudi shule na kuanzisha biashara ndogo. Katika changamoto zote, anasimama imara na kuwa mkombozi wa familia yake, hasa pale mumewe alipokosa mwelekeo. Ni hadithi ya ujasiri na matumaini, ikionyesha kuwa ushindi unaweza kupatikana hata kwenye mazingira magumu zaidi.
Maturity Level : all